November 4, 2019


OBREY Chirwa kiongozi wa safu ya ushambuliaji wa Azam yenye wakali wawili Donald Ngoma na Idd Seleman ‘Naldo’ leo wamepewa kazi ngumu ya kuipa pointi tatu mbele ya Kagera Sugar.

Azam FC ipo chini ya Kocha mpya, Arstica Cioaba alipoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0 leo atarusha kete yake ya pili mbele ya Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC Idd Cheche amesema kuwa wamegawa majukumu kwa washambuliaji wao wakiongozwa na Chirwa ili kupata matokeo chanya.

“Kwenye ligi kikubwa kinachotafutwa ni matokeo jambo hilo limetufanya tufanye kazi na safu ya ushambuliaji kwa kuwapa maelekezo mapya na majukumu mazito kushirikiana na wengine ili kupata ushindi.

“Kikubwa tumewaambia wawe watulivu wakiwa eneo la hatari na kufanya maamuzi kwa usahihi hivyo Chirwa, Ngoma na Naldo wana kazi ya kuwaongoza wachezaji wenzao kutafuta ushindi tunajua mchezo utakuwa mgumu,” amesema Cheche.


1 COMMENTS:

  1. Ngoma droo hakuna mbabe leo.but the time will tell lets wait.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic