JANA visiwani Zanzibar imechezwa fainali ya kombe la Karume Cup na timu ya Nyuki imekua bingwa kwa kuifunga timu ya Stone Town vikapu 78 kwa 75 dhidi ya timu ya Kichungwani.
Timu ya Blaze imekuwa ya tatu kwa kuifunga New west vikapu 75 kwa 52 kwa upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake A. Magic wamekua mabingwa K.V.Z mshindi wa pili na J.K.U mshindi wa tatu.
Jumla ya timu 19 zilishiriki michuano hiyo ambayo ilikuwa ni ya kukata na shoka mwanzo mwisho.
Karume Cup imeisha sasa ni maandalizi ya kombe la Wooter Afrika linalotarajiwa kuanza Desember 1.
0 COMMENTS:
Post a Comment