November 19, 2019

WAKALA wa kiungo anayekipiga katika klabu ya  Borussia Monchengladbach, Mathieu Beda amesema kuwa mteja wake Denis Zakaria  anaweza kuondoka kwenye timu hiyo mwezi Januari ndani ya Bundesliga na kuibukia Ligi Kuu England.

Zakaria mwenye mwenye miaka 22 inaelezwa kuwa uwezo wake umezivutia klabu kubwa nchini England ambazo ni Arsenal na Manchester United zinazohaha kuboresha vikosi vyao kwa sasa.

Timu zote za England zimeonyesha nia ya dhati na zipo tayari kuvunja benki na kutoa kitita cha pauni milioni 44 ili kuipata saini ya nyota huyo ambaye hana makuu akiwa uwanjani.

Kwenye jumla ya mechi 11 ambazo ameanza kiungo huyo amefunga jumla ya mabao mawili akitoa pasi moja ya mwisho na ameonyeshwa kadi nne za njano,  Beda anaamini Denis atafanya vema kwenye timu yoyote atakayokwenda kutokana na uwezo alionao.

Monchengladbach inaongoza Bundesliga ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 imeshinda mechi 8 ina sare moja na imepoteza mechi mbili ikiwa na pointi zake 25 kibindoni.
2 Attachments
 
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic