RASMI sasa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amepigwa chini ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na kile kilichoelezwa kimetokana na matokeo mabovu ya msimu huu ndani ya Ligi na mechi za Kimataifa.
Habari zimeelezwa kuwa leo Yanga imeachana na Zahera ambaye msimu uliopita aliongoza Yanga kucheza mechi 18 za Ligi Kuu Bara bila kufungwa mpaka ilipodondokea pua mbele ya Stand United uwanja wa Kambarage kwa kufungwa bao 1-0.
Nafasi yake kwa sasa inachukuliwa na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa, Charlse Boniface Mkwasa (Mkwasa Master) atakayekaimu kwa muda wa wiki mbili kabla ya kumpata Kocha Mkuu.
Maskini Mkwasa amepewa shipa ili ahukumiwe kwa makosa yasiyo yake. Ni heri akaikataa kazi hiyo na ikafanywa na mwenyekiti maana anayo sifa ya ukocha mahiri.
ReplyDeleteAtaondoka na Molinga au vipi?tunahitaji kujua
ReplyDeleteImekuwa poa sana.
ReplyDeleteDuh! Hapo bila kupepesa macho fimbo ya lawama inadondokea kwa Mkwasa master
ReplyDeleteZahera alitengeneza mwenyewe kuondoka kwake, akajenga kiburi kwamba hakuna wa kumfukuza, akawekeza kwenye kuongea ungedhan ni mwenza wa Haji!
ReplyDeleteAlifikia hatua eti anadai "anazo offer nyingi mkononi!"; huo ni uropokaji wa hali ya juu hata Mourinho alipofukuzwa alidai kuwa na offer nyingi mezani na hawezi kukosa kaxi lakin hadi leo hii anadanga.
Safari njema Zahera hope utajifunza kutokana na fursa hii.
Kwa Mkwasa, inaweza kuwa nafas nzuri sana kuinukia upya baada ya kutoka kwenye channel; hasa ukimtafuta Idd Cheche ili akueleze huwa anafanikiwa wapi kujenga timu, lakin pia nimuonye kazi ya ukocha hasa wa timu zetu hizi, si nzuri kwa watu wenye maradhi ya moyo.
Wabillah taufiq