November 2, 2019


Baada ya Pyramids kuifunga Yanga kwa mabao 2-1 pale CCM Kirumba asilimia kubwa ya mashabiki wamekata tamaa na kusema game imekwisha.

Kweli ni vigumu kuwafunga Warabu kwao lakini katika soka mambo mapya hutokea na rekodi kuandikwa.

Kwa sisi wa zamani, nakumbuka mwaka 2003 nikiwa mwandishi ninayechipukka kwa kasi, mjadala ulikuwa hivi, Simba licha ya kuifunga Zamalek bao 1-0 kwa bao la Emmanuel Gabriel basi safari ilishawakuta na kule Cairo watapigwa 5 au 6.

Mwisho Simba walifungwa 1-0 na game ikaenda kwenye penalti na mwisho Simba wakaivua Zamalek ubingwa wa Afrika... Huu ni mfano mzuri.

Yanga WANA NAFASI kwa kigezo KIMOJA tu, kuwa HUU NI MPIRA.

Fedha pekee haichezi, ukubwa pekee haushindi.

Lakini hauwezi kushinda hadi uamini UNAWEZA KUSHINDA.

Kama Yanga watacheza Misri wakiwa na hofu na kuamini mambo ya mashabiki basi kweli watafungwa na ikiwezekana kweli nyingi.

Lakini wakiamini inawezekana basi HAITASHINDIKANA. umeona kama ubora ni wa kutisha walikuwa nao Pyramids basi wangeshinda 4 pale Kirumba.

Yanga hawakuwa na approach nzuri katika mchezo wa Kirumba. Sasa wana nafasi nyingine na wana uwezo wa kufanya bora zaidi na hii inawezekana kabisa.

Soka ni mchezo wa makosa na ukirekebisha basi unaweza KUFANYA VEMA.

Bado Yanga ina kikosi kinachoweza kufanya jambo lakini hii lazima iingie katika MIOYO YA WACHEZAJI KWANZA.

Mashabiki waacheni waendelee na YAO nyie fanyeni KAZI YENU KWA UFASAHA na UFANISI... Kujituma ni lazima.

5 COMMENTS:

  1. Kaza maji kwenye gunia. Wakifungwa chache ni 4.Msiwajaze ujinga wachezaji.

    ReplyDelete
  2. pole bro,hawana timu chura na kumbuka yondani hachezi

    ReplyDelete
  3. J2 si kesho.endeleeni kujipa moyo

    ReplyDelete
  4. hayo ni maoni yake na yanapaswa kuheshimiwa,hata game kati ya yanga na town ship rollers wako waliyoibeza yanga na mwisho wa siku walishinga na wakafika hapo walipo,na timu zilizokuwa na nafasi ya kusonga mbele kama Simba na KMC Wakashindwa kufanya vizuri nyumban,so anything can happen

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic