November 2, 2019



ARISTCA Cioaba, raia wa Romania Kocha Mkuu wa Azam FC mwenye kandarasi ya mwaka mmoja anakabiliwa na mtihani wa pili kumenyana na Kagera Sugar maarufu kama Wanakulukumbi baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.

Novemba 4 Azam FC itamenyana na Kagera Sugar ikiwa ni mchezo wake wa sita utakaopigwa uwanja wa Azam Complex katika mechi tano imeshinda tatu na imepoteza mechi mbili ikijikusanyia pointi tisa kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddy Cheche amesema kuwa kupoteza michezo miwili mfululizo kumewapa somo watarekebisha makosa ili kupata matokeo chanya.

“Kushindwa kwetu kupata matokeo kwenye mechi  mbili msimu  mfululizo sawa na dakika 180 inatuumiza na inatufanya tutafute mbinu mbadala ya kutafuta ushindi kupitia makosa yetu tunaomba sapoti ya mashabiki indelee kuwepo,” amesema.

Msimu uliopita wa mwaka 2018/19 Azam FC iliifunga Kagera Sugar nje ndani ambapo mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0 uwanja wa Kaitaba na ule wa pili ilishinda mabao 2-0 uwanja wa Azam Complex. 


1 COMMENTS:

  1. ameshachapwa mara mbili kumbuka tangu akabidhiwe timu,amechapwa na simba na ruvu shooting,sasa unaposema kibarua cha pili tunashindwa kukuelewa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic