November 6, 2019


MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania mwenye umri wa mika 26 ameweka rekodi ya kuwa mtanzani wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga bao kwenye uwanja wa Anfield.

Samatta anayekipiga Genk ya Ubelgiji alimfanya Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp atabasamu kwa furaha licha ya bao kuzama nyavuni kutokana na uhodari wake wa kuruka angani mbele ya ukuta bora wa dunia mbele ya James Milner.

Bao lake hilo alilofunga dakika ya 40 linamfanya afikishe jumla ya mabao mawili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pia Samtta aliifunga Liverpool kwenye mechi ya kwanza bao la kichwa lilikataliwa na teknolojia ya VAR jambo lililomsikitisha mtanzania huyo pamoja na babaye mzee Ally ambaye alizimia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic