UONGOZI wa
Ndanda umesema kuwa kwa sasa tayari gari imewaka baada ya kuifunga mabao 2-0
Ruvu Shooting, watapambana kupata pointi tatu mbele ya Yanga kwenye mchezo wao
utakaochezwa Ijumaa uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ndanda
itaikaribisha Yanga, Oktoba 8 ikiwa na
joto la kupigwa chini kwenye michuano ya Kimataifa jambo ambalo linaongeza
uzito wa mchezo huo utakaokuwa wa tano kwa Yanga msimu huu.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Ndanda FC, Idrisa Bandari alisema kuwa
morali ya kikosi ipo juu na kikubwa ambacho wanakihitaji ni pointi tatu bila
kujali wanacheza na nani.
“Tunatambua
kwamba mchezo wetu ujao utakuwa dhidi ya Yanga tumejipanga kuona namna gani
tutabeba pointi tatu ili kuwa sehemu nzuri kwenye ligi kwani ligi imekuwa na
ushindani mkubwa,” alisema Bandari.
Ndanda FC
imecheza jumla ya mechi 8 imejikusanyia pointi saba zinazoifanya iwe nafasi ya
19 huku wapinzani wao Yanga wana pointi
saba nafasi ya 18 imecheza mechi nne pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment