November 6, 2019

MWINYI Zahera, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa aliwaambia viongozi wa Yanga wakamilishe malipo kwa wachezaji wote waliokuwa wanadai haki zao kutokna na kuitumikia timu hiyo bila malipo ikiwa ni pamoja na Vincent Andrew 'Dante'.

Zahera amesema kuwa miogoni mwa sababu zilizomfanya aje na wazo la kubwa kuliko ni pamoja na malipo ya wachezaji ambao hawakupewa stahiki zao.

"Wachezaji wengi walikuwa wanadai fedha nyingi na ilikuwa ngumu kwao kufanya mambo kwa usawa kutokana na uchumi kuyumba kwao jambo hilo limefanya Dante agome ilihali nilikuwa namhitaji.

"Ajabu ni kwamba baada ya kupata fedha wakaanza kusajili wachezaji wapya jambo ambalo halikuwa kwenye makubaliano yetu.

"Endapo Dante angekuwa hana haki ningemsimamisha jumla kama ilivyokuwa kwa Beno Kakolanya ili aendelee na maisha yake lakini nilishindwa kumuacha kwa kuwa alikuwa na haki," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Zahera ningekushauri unyamaze tu na kuwashukuru Yanga kwa kutokufukuza siku nyingi!
    Nina hoja kuu zifuatazo:
    1. Kutolipwa kwa madai ya wachezaji kunahusiana vipi na timu kukosa stamina na muunganiko?
    2. Mbona wachezaji wapya waliosajiliwa kwa mapendekezo yako; likiwemo bomu Molinga, ambao hawana madai, ndio wanaoongoza kwa viwango vibovu kiasi kwamba wengine umeshindwa kuwatumia kabisa? Tunahitaji pro wa kukaa benchi?
    3. Ni vipi kutolipwa kwa Dante na Juma Abdul kunahusika na kupanga timu vibaya, Balama kucheza beki au winga, kuchelewa kufanya sub hata inapoonekana kuhitajika, kupanga timu bila uwiano nk
    4. Ni vipi malipo ya wachezaji yanaibuka sasa wakati alituaminisha kila mara kwamba anaouzoefu wa kupindua meza?
    5. Ni vipi malipo ya Dante yanahusiana na yeye kugomea kupata Kocha Msaidizi, ambaye angekuwa msaada kwake kiufundi na mbinu?
    Zahera nyamaza kimya uende kishujaa ili angalau tukukumbuke kwa machache mazuri lakin kimbinu na ufundishaji umepwaya sana labda kiuhamasishaji na kuchonga (kuongea bila kiwambo)
    Aurevoir ci vou plait

    ReplyDelete
  2. mlipeni pesa zake Pondamali anadai, Dante na waxchezaji wengine wanadai morali ya wachezaji imeshuka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zingatia mada: hoja hapa sio kulipwa wala morali! Hoja ni sababu alizozitoa Zahera kuhusu timu kufanya vibaya, hakuna alipoelezea kutolipwa yeye kama sababu ya wachezaji kukosa muunganiko na stamina. Hakuna aliposema kuunga wingi moja au kuchezesha strika mmoja kulisababishwa na morali kushuka. Fungua macho na fikra

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic