November 28, 2019


Ukimuona mshambuliaji wa Simba Miraji Athuman ‘Sheva’ kwa sasa unaweza usimfahamu kirahisi kutokana na kubadilisha muonekano wa kichwa chake.

Sheva toka kuanza kwa msimu huu alikuwa anaonekana na nywele zilizosokotwa juu, lakini kwenye mazoezi ya Simba yaliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Gymkhana, ameonekana na staili mpya ya nywele.

Inaelezwa kuwa, Sheva ameamua kunyoa nywele hizo, kutokana na ushauri aliopewa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, wakidai kuwa mtindo wa awali ni wakihuni na hauendani na umri wake.

Championi Jumatano, lilipata nafasi ya kuzungumza na Sheva, ambaye alisema kuwa: “Nimeamua kunyoa hivi ili niwe na muonekano tofauti, hakuna jambo lingine.”

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic