STARTIMES YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MATATIZO YA MOYO MUHIMBILI
Kampuni ya Startimes kupitia chapa yake ya StarTimes leo,wametembelea watoto wenye matatizo ya Moyo katika Taasisi ya Moyo Muhimbili na kutoa mfano wa Hundi ya shilingi Milion 4 kwaajili ya mahitaji yao mbalimbali ikiwamo matibabu.
Startimes imetambua umuhimu wa kuwachangia watoto hawa kwa kutambua kwamba wengi wao wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo ,chakula,matibabu na hata mavazi,hivyo imeona ni vyema kushirikiana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz kuwafikia watoto hawa na kuwafariji.
"Huu ni mpango ambao kampuni ya Startimes imejiwekea kila Mwaka katika kuhakikisha inaifikia jamii kwa namna moja au Nyingine," Alisema Bw.David Malisa Meneja Masoko wa Startimes.
Katika kuhakikisha Wasafi Festival inafanikiwa Startimes tumeshiriki katika kuwezesha tamasha hili kama mdhamini wa Tamash, " laiongeza David Malisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment