STRAIKA SIMBA AJA NA TAMKO LA AINA YAKE
STAA mpya wa Simba, Athumani Miraji ‘Sheva’, ametamba kuwa bado hajaonyesha kiwango kile kikubwa anachokitaka yeye huku akiahidi kuifanyia makubwa timu yake hiyo mpya ikiwemo kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku moja mara baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kiungo huyo ambaye hakuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoivaa Prisons kutokana na majeraha, hadi sasa tayari amefanikiwa kufunga mabao manne huku akisababisha penalti tatu na ametengeneza asisti moja.
Sheva alisema anaamini bado ana imani kubwa ya kuendelea kuwatengenezea nafasi za kufunga wachezaji wenzake, pia yeye mwenyewe kufunga mabao kutokana na malengo aliyojiwekea.
Sheva alisema anafurahia ushirikiano mkubwa anaopata kutoka kwa wachezaji wenzake mara baada ya kutua Simba kwenye msimu huu wa ligi akitokea Lipuli FC ya Iringa.
“Kila mchezaji ana malengo yake aliyojiwekea, kama mimi baada ya kujiunga na Simba ninafikiria kuifanyia mengi mazuri ikiwemo kuipa ubingwa wa ligi na Kombe la FA, hivyo suluhu waliyoipata na Prisons siyo sababu ya wao kupoteza matumaini ya kutwaa mataji hayo.
“Hivyo, kama mshambuliaji nitapambana kuhakikisha ninatengeneza nafasi za kufunga, pia mimi mwenyewe kufunga mabao kwa kila nafasi nitakayoipata uwanjani.
“Ninafaurahia sapoti kubwa niliyoipata mara baada ya kujiunga na Simba, kwani nimekuwa nikipata pongezi nyingi na kupewa maneno ya kunipa wmoyo, hivyo ninajisikia furaha kuwa hapa,” alisema Sheva.
0 COMMENTS:
Post a Comment