Na Saleh Ally
MOJA ya mechi kubwa zaidi duniani ni pale Bayern Munich wanapokuwa wanakutana na Borussia Dortmund na hasa katika Ligi Kuu ya Ujerumani.
Kwa hapa nyumbani, ligi hiyo maarufu duniani inaonyeshwa moja kwa moja kupitia king’amuzi cha StarTimes.
Sifa kuu ya king’amuzi cha Startimes pamoja na kuleta burudani hiyo pia kinasifika kwa ubora wa mwonekano kwa kiwango kikubwa kabisa hasa kupitia High Definition maarufu kama HD.
Ligi hiyo maarufu ni kati ya ligi chache zinazosifika kuwa na timu bora, wachezaji mahiri lakini ubora wa juu katika suala la takwimu.
Takwimu za Bundesliga zinaonyesha zaidi ubora wa soka kwa maana ya mashuti langoni, mengi yaliyolenga, ubora wa pasi, asilimia juu ya zilizofika, nafasi zilizotengenezwa na nyingi zilizotumika na kadhalika.
Wakati utakuwa ukipata hayo katika Bundelisga, mechi hiyo ya Jumamosi ni habari nyingine. Itakuwa kwenye dimba la Allianz Arena, Munich maarufu kama Bavarians wakiwa nyumbani lakini wakijua wana deni kubwa kwa mashabiki wao.
Hadi sasa hawajakaa vizuri kutokana na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Eintracht Frankfurt, jambo limesababisha kufukuzwa kwa kocha wao Niko Kovac kufutwa kazi.
Tokea amefukuzwa Kovac, Munich wameshinda mechi moja dhidi ya Olympiakos Piraeus ambayo walifunga mabao 2-0, jambo ambalo kwa mashabiki wanalichukulia kama nafuu na si uhakika.
Swali la kama wamerejea katika kiwango cha kuweza kupewa heshima na mashabiki wao kwa kusahau yale ya Munich, litajibiwa keshokutwa Jumamosi.
Hofu ni kwamba Bayern bado hawajakaa vizuri katika msimu huu licha ya kuwa na uzoefu mkubwa na ukubwa wa muda mrefu katika Bundesliga.
Katika mechi 10, wameshinda tano tu, sare tatu na wamepoteza mbili. Sasa wako katika nafasi ya nne wakikutana na Dortmund ambao wako katika nafasi ya pili baada ya kushinda mechi tano pia, wakitoka sare nne na kupoteza moja.
Unaweza kusema watu wazima kama wote hawako vizuri sana, hivyo kila mmoja anaweza kutaka kuamkia kwa mwenzake hiyo Jumamosi.
Mechi nne za ugenini zinaonyesha Dortmund nao hawakuwa vizuri kwa kuwa walishinda moja tu na kutoa sare tatu lakini Bayern wao katika mechi za nyumbani wamekuwa na nafuu ingawa walipoteza dhidi ya Hoffenheim wakiwa nyumbani pia.
Itakuwa ni mechi ya vigogogo wanaitaka kuamka, kila mmoja akionyesha ana nia ya kuweka heshima kwa mashabiki wake.
Inawezekana na Startimes wamekuwa wakisisitiza kwa wale ambao hawajalipia ving’amuzi vyao kuamka na kupambana kulipa ni Sh 18,000 tu.
Burudani hii si ya kukosa, nani atainuka, itakuwaje na nani ataanguka. Ni Jumamosi kwenye Startimes moja kwa moja kutoka jijini Munich kwenye dimba la Allianz Arena.
0 COMMENTS:
Post a Comment