November 9, 2019

OLE Gunnar Solskjaer, Meneja wa Manchester United amewataka wachezaji wake kuongeza morali na kucheza kwa kujituma kwenye mechi zao za Ligi Kuu England ili kupata matokeo chanya.

United haijawa na mwenendo mzuri ndani ya Ligi Kuu England kutokana na kupata ushindi kwa tabu ndani ya ligi msimu huu ikiwa nafasi ya 11.

Imecheza mechi 11 imeshinda tatu pekee huku ikilazimisha sare mechi nne na kutoa sare mechi nne na ina pointi 13.

"Nahitaji kuona wachezaji wanajituma kwenye ligi kwa kufanya mambo makubwa ambayo yatatupa matokeo chanya, imani yangu kila kitu kinawezekana na ni muhimu kujituma," amesema.

Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Brighton utakaopigwa kesho uwanja wa Old Traford Novemba 10 ambayo ipo nafasi ya 8 ina pointi 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic