PATRICK
Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa alistahili kupata sare ya bila
kufungana na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kutokana
na kikosi hicho kuwa na mbinu za kiufundi mwanzo mwisho.
Simba ambao
ni mabingwa watetezi wa ligi Novemba 7 ilikubali kupata sare ya bila
kufungana na Prisons kwenye mchezo wake wa tisa wa ligi uliochezwa uwanja wa
Uhuru.
Aussems
amesema kuwa Prisons ilifanikiwa kuwa na ukuta mgumu ambao ulikuwa ukizuia
mipango ya wachezaji wake wa Simba na ilikuwa ikifanya mashambulizi ya
kushtukiza na kurejea kwenye nafasi zao kwa wakati kwa kila mchezaji.
"Kazi kubwa ambayo wachezaji walikuwa wakifanya ilikuwa ni kupambana na timu ambayo ilijipanga kujilida na kushambulia kwa kushtukiza jambo ambalo limetufanya tusipate ushindi.
"Nawapongeza wapinzani wetu kwa kupambana na kupata sare licha ya wachezaji wangu kupambana kutafuta ushindi, ni wakati wetu kujipanga kwa ajili ya wakati mwingine," amesema.
Sare hiyo
inaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 22 ikijikita kileleni huku Prisons
ikiendeleza rekodi yake ya kutokupoteza mchezo ndani ya ligi baada ya kucheza
mechi 10 ikiwa na pointi 16 imetoa sare mechi saba na kushinda mechi tatu
inashika nafasi ya nne kwenye msimamo.
0 COMMENTS:
Post a Comment