November 16, 2019


Taarifa za ndani zilizopo kutoka Young Africans zinasema kuwa mabosi wa timu hiyo wanaweza wakaachana na wachezaji wake watatu wa kimataifa.

Zoezi hilo linaweza kukamilika ndani ya dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa rasmi kwa timu husika kutumia kipindi hiki kusajili wachezaji wapya ili kuboresha vikosi vyao.

Habari za ndani zinaeleza Yanga inaweza kuachana na Maybin Kalengo, Mustafa Seleman pamoja na Issa Bigirimana ambao inatajwa kuwa hawajaonesha kile ambapo kilitarajiwa na wengi.

Licha ya taarifa hizo kuwepo, imekuwa ikielezwa Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa, amedai atahusika katika kupunguza baadhi ya wachezaji ambao anaona hawana msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic