November 14, 2019


Baada ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kumteua aliyekuwa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, inaelezwa kuwa atakabidhiwa majukumu ya kusimamia suala la VAR (Video Assistant Referee).

Wenger ametangazwa jana na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka Duniani, wadhifa ambao umekuja tangu aachane na Arsenal.

Taarifa zinasema katika majukumu ambayo Wenger atakuwa nayo ni pamoja na kusimamia suala la VAR ambayo imekuwa gumzo zaidi duniani kwa sasa.

Kocha huyo wa zamani atahusika na kuratibu mambo mbalimbali ikiwemo kuangalia mapungufu ya VAR na kufanya maboresho pale ambapo itatokea.


  


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic