ZAHERA AINYIMA UBINGWA SIMBA, SABABU AZIANISHA HADHARANI
WAKATI bado akiwa kwenye presha ya kufukuzwa, kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa haoni dalili za wapinzani wao Simba kuchukua tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huku akienda mbali zaidi kwa kusema anajua atamalizia wapi watapokutana.
Simba wanaongoza ligi ikiwa na pointi 21 ikipoteza mchezo mmoja pekee wakati Yanga ipo katika nafasi ya 17 ikiwa
na pointi saba baada ya kucheza mechi nne ikishinda mbili, sare moja huku mchezo mmoja ikipoteza.
Akizungumza na Spoti Xtra nyumbani kwake kabla ya kwenda Misri, Zahera alisema kuwa ana uhakika kwa Simba ya msimu huu haitoweza kuchukua ubingwa licha ya kufanya usajili mkubwa.
“Ligi ya msimu huu ni ngumu kwa kweli, kila timu inajaribu kuonyesha ushindani, binafsi sioni dalili za Simba kutetea ubingwa wao kwa mara tatu, hilo halitowezekana kutokea kwa sababu ukiangalia kila timu inajitahidi kupambana.
“Kushinda mechi nyingi katika ligi ambayo bado haijafika mbali haliwezi kuwa suala ambalo linaweza kuwapa ubingwa kwa sababu huu ni msimu mwingine kila kitu kimebadilika na hata tutakapokutana nao wajue itakuwa tofauti kwani nimeshawajua vizuri mambo yao,” alisema Zahera
CHANZO: SPOTI XTRA JUMAPILI








Sasa bora ushughulikie kulinda kibaruwa chako kwani uwezo duni wa wachezaji tuliouona Jana ni wakuvunja moyo. Ulifikirie hilo kwanza kabla ya kufikiria kuwanyima Simba ubingwa kwani tulichokishuhudia Jana ni wachezaji kuchezeshwa kindumbwendumbwe toka mwanzo mpaka mwisho
ReplyDeleteBooo Zahera hizo ni ndoto za mwenda wazimu.Simba is the next level 10 years back to back.Sisi Simba tunakuachia Masawe Bwire tu
ReplyDeletehata mwaka jana wakati simba ina viporo sita na Yanga imebakiza mechi tatu alikuwa anaamini Simba haitakuwa bingwa
ReplyDeleteYako yanakushinda umeishia kufungwa magoli 5 utayaweza ya simba?
ReplyDeleteBoooo
ReplyDeleteDaah! ama kweli Zahera umenichekesha sijui umenishangaza!
ReplyDelete