November 4, 2019


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema kuwa malengo yao msimu huu ni kufikisha alama 100 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Manara amesea hayo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pyramids FC katika mchezo wa ligi jana dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Manara ameeleza kuwa wanatamani kufikisha alama hizo ili kuweka rekodi ya aina yake japo akikiri si rahisi sababu kila timu ina malengo ya kupata matokeo.

"Msimu huu tuna malengo ya kufikisha alama 100 kwenye ligi ili kuweka rekodi ya aina yake.

"Najua ligi ni ngumu na kila timu inapanga kushinda hivyo lazima tukutane na changamoto, Simba haiwezi kushinda kila kitu."

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic