ZAHERA ATOA TAMKO JUU YA MADAI YA WACHEZAJI YANGA KUHUSISHWA NA USHIRIKINA
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuhusiana na baadhi ya madai ya wachezaji kujihusisha na ushirikina.
ahera amefunguka hayo wakati akihojiwa na gazeti la Championi kufuatia kuwepo kwa tetesi hizo kuwa ushirikina umekuwa ukichukua nafasi ndani ya kikosi kwa baadhi ya wachezaji kwa kufunguka yafuatayo:
Swali lilikuwa hivi: UNAZUNGUMZIAJE MADAI YA WACHEZAJI WAKIKIMBIA KUCHEZA NAFASI YA JUMA ABDUL KWA KUWA WANAUMIA WAKIHUSISHA NA USHIRIKINA?
“Ni kweli alicheza Mapinduzi aliumia lakini sikuweza kumtumia Juma Abdul kwa kuwa alichelewa kwenye maandalizi ya msimu kutokana na matatizo yake na uongozi akiwa na Dante.
“Sasa wakati anakuja Morogoro sisi tulikuwa tumeshamaliza maandalizi yeye ndiyo akawa amekuja lakini hakuwa anacheza kwa kuwa hakuwa fiti kabisa tofauti na wenzake lakini tulivyokuwa Mwanza ambapo nilipanga kuanza kumtumia ndiyo akapatwa na msiba wa mama yake, akaondoka.
“Nilimchukua katika safari ya Zambia kwa ajili ya kukamilisha idadi lakini siyo kucheza kwa kuwa bado hakuwa sawa na siyo kweli kwamba wachezaji walikuwa wakiogopa kucheza kwenye nafasi hiyo,” anamalizia Zahera.
CHANZO: CHAMPIONI








Kumtoa Makame kulifanya beki ielemewe hata alipoingia Fei alikuwa hana ubavu na kimo cha urefu kupambana kwa mipira ya katikati, na matokeo yake Lamine na Ali Ali kutumia nguvu nyingi mwishowe kusababisha kuumia...bado benchi la ufundi limeendelea kufanya makosa kwenye substitutions...kwa mara nyingine. Kulikuwa hakuna haja ya Kumtoa Balinya timu ilishindwa kushambulia....Sadney alionekana peke yake kule mbele
ReplyDeletesijaelewa hii
ReplyDeletemtu ambaye alikuwa atoke ni shishimbi. Hakuwa na perfomance.
ReplyDeleteTshishimbi atatokaje nä yeye mcongo kama Zahera.
ReplyDeleteDawa ya Mgonjwa ni kufanya upasuaji ili kuondoa kiini cha ugonjwa sio kumpatia chakula ukitegemea kiini kitaondoka....Tatizo ni benchi la ufundi limefikia ukomo wa uwezo hiki ndicho chanzo cha mashabiki kushinikiza kuondolewa kwa Kocha au Mabadiliko kufanyika. Hata ukisajili akina Messi na Ronaldo kama ufundishwaji ni poor usitegemee ushindi. Yanga hii inahitaji uwekezaji bora ambao unaendana sambamba na benchi la ufundi lililo bora....Uongozi wa Yanga unajivutavuta na kujificha kwenye kichaka na kivuli cha Zahera lakini ukweli ni kuwa Kocha huyu hatawafikisha popote....mbinu zimegota...
ReplyDelete