ZAHERA: TUNAFANYA KOSA KUBWA WENYEWE
Kupitia gazeti la Championi Ijumaa, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aliishia kueleza mikakati yake katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri ambao utapigwa kesho Jumapili.
Zahera anaendelea kufunguka mambo mengi mazito juu ya mchezo huo na mambo mengine yanayoendelea kwenye timu hiyo.
“Unaweza kulalamika kwa timu ya Rwanda au Burundi, inakuja hapa inakufunga, inakutoa, lakini huwezi kulalamika na Pyramids kwa sababu unacheza na wachezaji wanaojitolea, wanaonyesha kwamba hawakuwa wabovu.
“Lakini tunafanya kosa kubwa wenyewe wanatuadhibu, ukiangalia wakati tunasajili hatukuwa na mipango ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatukuwa na mipango ya kusajili wachezaji kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa zaidi walikuwa ni kucheza ligi yetu."
Zahera una kaili nyingi sana
ReplyDeleteUmesema ana akili sana au kinyume chake?
ReplyDeleteTatizo hapa siyo ushindi bali timu aliyousajili kwa ajili ya ligi ya hapa, haina muunganiko, haichezi kama timu na hata hao mapro aliowasajili wengine bado hawajatumika. Timu hii haijavutia hata kwenye ligi yetu ikicheza mchezo mbovu kabisa, atuambie alisajili timu kwa mashindano yapi labda ya taarabu au bongo star search!