PATRICK
Aussems, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgij amesema kuwa tatizo kubwa
linalowafanya wachezaji wake washindwe kucheza soka la darasani ni ubovu wa
baadhi ya viwanja wanavyotumia.
Mbelgiji
huyo amesema kuwa ni ngumu kwa ligi ya Bongo kuendelea iwapo tatizo la viwanja
litafumbiwa macho kwani mchezaji bora anatengenezwa kwenye mazingira makini.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa lengo kubwa la timu yake ni kuona inashinda
mechi zake zote licha ya ugumu wa viwanja vilivyopo.
“Maendeleo
ya mpira yanahitaji uwekezaji na kupata matokeo wakati mwingine kunategemea na
uwanja ambao wachezaji wanacheza ila kwa hapa kuna tatizo kwenye viwanja vingi
kutokuwa kwenye ubora jambo ambalo linaua utamu wa soka.
“Haijalishi
tunacheza uwanja gani kikubwa ambacho tunakitazama ni matokeo chanya, ushindani
ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tutapambana kupata atokeo chanya
kwenye mechi zetu,” amesema Aussems.
Miongoni mwa
viwanja ambavyo Simba imevitumia msimu huu ni pamoja na kile cha Karume, Mara
dhidi ya Biashara United, Sheikh Amri Abeid dhidi ya Singida United, Kambarage dhidi ya Mwadui ambavyo
Mbelgij alidai kuwa ubora wa uwanja ulikuwa hafifu.
UKIFUNGWA KUBALI TU ACHA VISINGIZIO MANA KAMA VIWANJA NDO MIAKA YOTE TUNAVITUMIA TATIZO LENU MIKIA LA KUMALZA MANENO YANGA WAMEFUNGWA NA RUVU MUKASEMA KOCHA ZAHERA MBOVU LEO MUMEKANDAMIZWA MBONA HAMUSEM AUSEM MBOVU NA WALIMA VIAZ NA MADN MUNALETA MAMBO YA AJABU KUPGWA MUMEPGWA TU MUKUBALI MATOKEO MIKIA.
ReplyDeleteAussems hakatai kufungwa kwani matokeo ya mpira ni kufunga,kufungwa na kutoka sare.Hata msimu wa ligi uliopita pia kocha wako huyo papa zahera alilamikia sana ubovu wa viwanja.Licha ya wachezaji kutocheza mpira wanavyo elekezwa na makocha wao lkn pia inachangia sana majeruhi kwa wachezaji.Ushauri wangu TFF waendelee kuvifungia viwanja vibovu.
DeleteVyura kama mlivyobatizwa Sasa "malalamiko FC"hamueleweki maana Simba ikishinda mechi refa ameibeba Simba mara Simba imetoa rushwa kwa TFF.Ikifungwa Simba basi ni halali yao.Kocha Aussems ametoa tathmini yake ya mchezo na hata timu take inaposhinda kwenye viwanja vibovu bado anabilalamikia kama alivyosema viwanja vya Karume (Musoma) na Arusha vilivyo vibovu.
DeleteChura soma kwa makini o be pyramid wàmekuchanganya
ReplyDeleteUsihangaike na kandambili kaka acha kesho wakapakatwe na waarabu warudi hao na ss lazima tuwapakate tu ni wetu THIS IS SIMBA
ReplyDeleteNaungana na Professor Aussems, tatizo la viwanja ni kubwa sana. TFF lazima ifanye kitu. Viwanja vyenye ubora tu ndio vitumike. Kama unadhani Simba ilizidiwa na Mwadui FC subiri uone watakapocheza Dar kwenye uwanja wenye viwango.
ReplyDelete