December 8, 2019

BONDIA wa ngumi za kulipwa za uzito wa juu, Anthony Joshua amefanikiwa kumtwanga mpinzani wake wa karibu Andy Ruiz Jr kwa pointi kwenye pambano lililopigwa kwenye uwanja wa Ad Diriyah, mjini Saudi Arabia usiku wa kuamkia leo.

Pambano hilo la uzito wa juu lilikuwa la marudiano na mabondia hao walikuwa wanawania mikanda ya WBA, IBF na WBA iliyokuwa mikononi mwa Ruiz Jr ambaye aliitwaa baada ya kumtwanga Joshua raundi ya Saba kwenye pambano la awali lililopigwa Juni, Mosi mwaka huu.

Ushindi huo unamfanya Joshua ambaye ni namba tatu kwa ubora duniani kwa ngumi za uzito wa juu kurudisha mikanda yake yote mitatu aliyoipoteza wakati alipochapwa kwenye pambano la awali na Ruiz Jr maarufu kama kibonge mwepesi.

Pambano hilo lililokuwa la raundi 12, Joshua alipata jumla ya pointi 118 huku Ruiz Jr akijipatia jumla ya pointi 110.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic