December 9, 2019


Jina la aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems limeibuka katika sherehe za uzinduzi wa uwanja wa Simba Bunju jijini Dar es Salaam juzi baada ya wachezaji wa timu hiyo kuonyesha bado hawataacha kumkumbuka kwa mambo aliyowafanyia.

Wakizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi mdogo wa uwanja huo wa kisasa ulihudhuriwa na mamia ya mshabiki wa klabu hiyo, walisema Aussems viwango bora walivyonavyo ni matokeo yaa kazi nzuri aliyoifanya kocha huyo kabla ya kutimuliwa kwa utovu wa nidhamu.

Claotus Chama

Kiungo huyo wa kimataifa wa Simba,alisema,kwa upande wake alisema, huwa anafurahishwa na kocha yoyote ambaye atakutana naye ndani ya klabu anayeweza kumjenga na kumuongezea ufanisi, hivyo kwa upande wa Aussems kuna kitu ambacho alimuongezea ubora alionao.

Mimi ni mchezaji wa muda mrefu nimeshakutana na makocha wengi, lakini Aussems kuna kitu kaniongezea naweza kusema nitamkumbuka sana, kilimchokumba kinaweza kutokea kwa yoyote kwa kwenye mambo ya kazi, wacha tuendelee kuheshimu maamuzi viongozi wetu,” alisema Chama.

Tairane Santos Da Silva

Beki huyo Mbrazil anasema, mazoea ni kitu kikubwa katika maisha lakini kila jambo lina wakati wake,hivyo kuondoka kwa Aussems ni wakati wake umefika lakini wamepata nafasi ya kuchota mazuri mengi kutoka kwa kocha huyo.

ìKila mmoja anaweza kusema yake, lakini binafsi naangalia kipi amenifanyia, kweli tulimzoea sana kocha, ila kila mwanadamu ana upungufu wake, zaidi tunamuombea mazuri aendako, mchezaji na kocha ni kitu kimoja, inawezekana tukakutana huko mbele ya safari,îalisema Santos

John Bocco

Nahodha wa Simba alisema, siku zote mchezaji huwa anapenda akaye na kocha kwa muda mrefu ili kuzoea zaidi mfumo wake, kwa upande wake Aussems amemuachia elimu nzuri ya Soka, hivyo atamkumbuka kwa mema yake, hata hivyo milima ndio haikutani lakini binadamu muda wowote wanaweza kukutana.

ìSiwezi kusema mengi sana, ila kocha alikuwa mzuri na amejitahidi kutufundisha mambo mengi, lakini mchezaji hachagui mwalimu, hata atakae kuja leo nae tutazoea mazingira yake na kazi itaenda, alisema Bocco.

Na Mwamvita Mtanda

1 COMMENTS:

  1. Dada mwandishi tumeshampotezea Kocha Aussems na imeshakuwa historia na maisha yanaendelea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic