Kiungo wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, amekanusha tetesi zinazomuhusisha na kazi ya kukinoa kikosi hicho, akisema akili yake iko kwenye kibarua chake cha sasa kwa ‘asilimia 300’.
Vieira ni kocha wa Nice ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) lakini amekuwa akitajwa kunukia Arsenal tangu Unai Emery alipofungashiwa virago wiki iliyopita kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi hicho.
“Sina cha kuzungumzia,” alisema Vieira na kuongeza: “Nina mambo mengi ya kufanya hapa (Nice) na sitaki kujivuruga kwa kitu chochote.”








0 COMMENTS:
Post a Comment