December 1, 2019

LICHA ya Edward Songo wa JKT Tanzania kupachika bao la kuongoza dakika ya 12 mbele ya Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Bara wameishia kuambulia pointi moja na kupata sare ya kufungana mabao 2-2.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Chamazi ulishuhudiwa bao hilo likisawazishwa na Agrey Moris dakika ya 79 kwa mkwaju wa penalti.

Kabla ya mpira kuisha, Danny Lyanga alipachika bao la pili dakika ya 86 kwa JKT Tanzania kabla ya Idd Seleman kusawazisha dakika ya 88.

JKT Tanzania inalazimisha sare ikiwa ugenini ikiwa na kumbukumbu za kufungwa mabao 3-2 na Yanga huku Azam FC ikitoka kushinda mabao 5-0 mbele ya Alliance FC.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic