PIERRE Aubameyang ameonyesha maajabu leo ndani ya kikosi chake cha Arsenal ameokoa jahazi kwa kupachika mabao mawili wakati timu yake ikimenyana na Norwich City.
Norwich ilianza kupachika bao la kwanza kupitia kwa Teemu Pukki dakika ya 21 kipindi cha kwanza lilisawazishwa na Aubameyang dakika ya 29 kwa mkwaju wa penalti ambao alikosa mara ya kwanza kabla ya VAR kuamua arudie na kufunga.
Dakika ya 45+2 Todd Cantwell alipachika bao la pili na kuifanya Arsenal kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma Kwa mabao 2-1.
Dakika ya 57 Aubameyang alifunga bao la kusawazisha na kufanya ngoma ikamilike kwa sare ya mabao 2-2.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa kaimu Kocha wa Arsenal Freddie Ljungberg kukaa benchi akipokea mikoba ya Unai Emery ikiwa ni mechi ya nane kwa Arsenal kucheza bila ushindi.
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kuwa nafasi 8 ikiwa na pointi 19 huku Norwich ikiwa nafasi ya 19 na ina pointi 11.
0 COMMENTS:
Post a Comment