Waswahili wanaweza kumtupia Senzo mzigo wa lawama. Bodi ya wakurugenzi ndiyo iliyofanya maamuzi, sio Senzo. Hakuna umoja ndani ya timu, timu imegawanyika. Tumefanya maamuzi ili kurekebisha hii hali. Timu ilikuwa inashinda kwa sababu ya uwezo binafsi wa wachezaji.
Viongozi hawakai na wachezaji kambini. Wajibu wa viongozi ni kuwaonya wachezaji na makocha kama kuna shida. Utovu wa nidhamu umekithiri, viongozi wamejitahidi lakini tabia hiyo inajirudia. Maamuzi haya ni kwa sababu kocha ameshindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji
Aussems amewagawa wachezaji makundi makuu mawili. Sasa kocha huwezi kuendesha timu hivyo. Juzi ametoka kumdhihaki mchezaji (Dilunga) bila sababu yoyote.
Wapo wanaodhani waliofanya uamuzi huu hawaipendi Simba. Sio kweli, yaani Mo Dewji haipendi Simba? Bodi ya wakurugenzi hawaipendi Simba? Haiwezekani Mo Dewji awekeze fedha zake halafu afanye maamuzi yasiyo na tija. Kama timu haina nidhamu haiwezi kusonga mbele.
Imeandaliwa na Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba
Maamuzi ya Simba ya kumtimuwa Ausems ni sahihi kabisa tena wamechelewa kuchukua maamuzi na wala hakuna haja ya uongozi wa Simba kutumia nguvu kubwa kuueleza umma kwanini wamemtimua kocha ila nguvu kubwa sasa kwa Simba ni kumleta mbadala wa Ausems aliekuwa bora zaidi kwisha habari.
ReplyDeleteMie wala siungi mkono hayo maamuzi ya bodi,kocha kumdhihaki mchezaji uongozi wana maana gani,wametupa maelezo ya upande mmoja lakin hatujasikia mwali kaongea nini,lakin shutuma zote zinamuendea mwalimu na ndio wameamua kumtoa kafara ili wao maisha ya kupiga hela za MOo ziendelee
DeleteAlipaswa kutimuliwa pale ilipotolewa raundi ya kwanza. Mimi iliniuma sana
ReplyDeleteUkweli Simba tokea ilipotolewa na UD Songo ikapoteza mwelekeo na tactical performance imeshuka.Ukipenda kujiridhisha angalia video clips tokea Simba day walipocheza na Power Dynamos,Azam(ngao ya jamii) Hadi mechi ya majuzi dhidi ya Ruvu.Ni dhahiri Kocha Aussems alikuwa ameishiwa mbinu na timu imekuwa ikicheza zaidi show game.Timu pinzani nyingi zimeshaijua uchezaji wa Simba na pale wanapoamua kupaki bus hapo kocha wetu Aussem anabaki kushika shavu asijue jinsi ya kutafuta mbinu mbadala na mfano mzuri wa mechi za Prisons,Mwadui,Bandari,Mashujaa, Aigre Noir nk.
ReplyDeleteMie naunga mkono viongozi wa Simba kwa uamuzi waliochukua wa kuachana na kocha Aussems lkn wanatakiwa kuleta kocha bora zaidi yake.
Kwani timu pinzani ikipaki bus kunakua na mbinu gani hebu tueleze?
Delete