December 17, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga upo katika hatua za mwisho za kumalizana na mabosi wa Azam FC juu ya kumsajili straika machachari Ditram Nchimbi.

Nchimbi ambaye anaichezea Polisi Tanzania kwa mkopo amekuwa akitajwa kutua Yanga ambayo imekuwa ikimuwinda kwa muda mrefu.

Inaelezwa kuwa Yanga wameshaweka milioni 20 za kitanzania kwa ajili ya kumchukua straika huyo ambaye amekuwa kwenye fomu ya aina yake.

Taarifa za ndani zinasema mazungumzo yanaenda vema na muda wowote Nchimbi anaweza akatangazwa kunako moja ya wakongwe hao wa Ligi Kuu Bara.

Wakati Yanga wakiwa wanapambana kumpata Nchimbi, dirisha dogo la usajili limefunguliwa jana ambapo timu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili zinaruhusiwa kufanya usajili.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic