December 16, 2019


LAMINE Moro, beki wa Yanga ambaye aliondoka hivi karibuni kutokana na madai ya mshahara na kurejea nchini Ghana inaelezwa kuwa amerejea Bongo kumalizana na mabosi wake hao.

Moro alikuwa bora kwenye mechi zake ambazo alizicheza akiwa na Yanga msimu huu.

Habari zinaeleza kuwa tayari amemalizana na Yanga ambao wanatarajia kucheza na Simba Januari 4 mwakani.

Moro alihusishwa kutua ndani ya Simba ambao walifanya naye majaribio na kuamua kumuacha na ilielezwa kuwa alikuwa anahitajika kwa sasa ili akaitumikie klabu hiyo yenye maskani yake Kariakoo.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alisema kuwa Moro bado ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa bado anamkataba ndani ya timu hiyo.

7 COMMENTS:

  1. Hamlipi mpaka mgomewe na kukimbiwa halafu mnalipa kuwaogopa wanamsimbazi na hiyo iwe silaha yenu kali ya kudai na kulipwa kwakutishia kuhamia Msimbazi

    ReplyDelete
  2. nani akikuambia simba ilikua namtaka hivi kwa hapa bongo kuna mchezaji anaweza takiwa simba kwa sasa akagoma sema alikua anadai chake mfano ajib, kakoranya hao walitakiwa uliona kilichotokea

    ReplyDelete
  3. Hahahahaha lini Simba walimtaka huyooo
    Yy na mwenzie yulee Urikhob walifeli kwenye majaribiooo
    Na km simba wangemtaka asingechomokaa

    ReplyDelete
  4. Wanatiana saini kama vile mchezaji mpya kwasababu Hakuna kuaminiana

    ReplyDelete
  5. Kila pesa kuna jinsi ya kuipata. Pesa ya Yanga hata mshahara tu lazima simba itajwe ndipo ulipwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic