Bosi wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa, amesema kuwa zoezi la usajili ndani ya klabu hiyo haliwezi kufanyika bila mapendekezo ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck. Imeelezwa.
Taarifa imesema kuwa Mazingisa amefunguka hilo kutokana na majukumu hayo kuachiwa Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji kwa ajili ya dirisha dogo.
Katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni, uongozi wa Simba ulisema kuwa tayari wameshatenga bajeti ya usajili ndani ya dirisha dogo ambayo ni shilingi milioni 76 za Kitanzania.
Mazingisa ameeleza kuwa fedha hizo zitatumika tu endapo Vandenbroeck ataona kama kama kuna haja ya usajili kufanyika ama la.
0 COMMENTS:
Post a Comment