Chelsea wataruhusiwa kusajili wachezaji katika dirisha dogo la usajili la Januari, baada ya adhabu ya kufungiwa na Fifa kupunguzwa kufuatia rufaa iliyokatwa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo CAS.
Chelsea walifungiwa kusajili kwa madirisha mawili ya usajili na Fifa mwezi Februari baada ya kukiuka sheria za usajili kwa wachezaji chipukizi.
CAS imepunguza adhabu hiyo kwa nusu na hivyo inamaanisha Chelsea tayari wametumikia adhabu yao katika dirisha la usajili lililopita.
Pia CAS imepunguza faini waliyotozwa Chelsea kutoka pauni 460,000 hadi 230,000.








0 COMMENTS:
Post a Comment