SAA,
dakika, sekunde zilikuwa zinakatika taratibu huku kila mmoja akihoji ni nini
ambacho kinapikwa ndani ya Simba na hakuna aliyekuwa anajua.
Ikawa
wiki, mwezi, miezi na hatimaye miaka ikakatika bila wale ambao walikuwa
wanapiga porojo kuhusu kukamilisha ndoto za uwanja kutimia zaidi ya kuwahadaa
wapiga kura.
Tumeona
ilikuwa ni wimbo wa muda mrefu kwa kuwa Simba ni miongoni mwa timu kubwa ambazo
zinafanya vema na kuleta ushindani kwa ukanda wa Afrika Mashariki inaweza
ikasonga mpaka na Kati kwa kuwa ina makombe kadhaa ya Cecafa.
Kila
mmoja mpenda maendeleo alikuwa anajiuliza kuna nini ambacho kinatokea ndani ya
timu hiyo ambayo ina wanachama lukuki na wanapenda maendelo ila hakukuwa na
majibu sahihi kwa wakati huo na kila aliyekuwa anapita alikuwa na stori zake
maisha yakaendelea.
Hata ilipobadilisha mfumo bado
kulikuwa na sarakasi za hapa na pale juu ya muda kamili wa kukamilika uwanja
baada ya timu kuwa mikononi mwa bodi ya wakurugenzi pamoja na wanachama wa
Simba,
Hii
ilikuja baada ya kubadili mfumo na kuweka kuwa kwa mfumo wa hisa uwekezaji wa
kisasa ambao umebarikiwa na Serikali.
Pale
Bunju nje kidogo wanaita ya jiji la Dar
ndio sehemu yao ambayo wameamua kujenga uwanja wa kisasa na umepewa jina la Mo
Arena Complex.
Katika
hili Simba mnapaswa pongezi kwa kuwa mmefungua njia ambayo ilikuwa imefungwa
kwa muda mrefu na hakukuwa na mwingine wa kuifungua zaidi yenu wenyewe kuamua
kuifungua.
80
ni namba ya kawaida ila unapokuja kuiweka kwa upande wa miaka ni mingi na si ya
kitoto kwani kama kungekuwa na mfumo bora ilitakiwa ujengwe uwanja mkubwa zaidi
ya ule wa Mo Arena.
Nakumbuka
kuna siku nilikuwa uwanjani natazama mechi ya Simba wakati ule wa Patrick
Aussems kwenye michuano ya kimataifa walikuwa wanacheza na AS Vita.
Mashabiki
wa AS Vita walipoona uwanja wa taifa umejaa na rangi ni nyekundu na nyeupe
walihofia na kuuliza hivi hawa ni mashabiki wa Simba na wameamua kuukomoa
uwanja wao kwa kuujaza namna hii?
Imani
yao walitambua kwamba kwa kuwa wapo ugenini na Simba ni jina kubwa basi hata
uwanja ule wa taifa waliamini ni wa Simba mpaka walipokuja kutambua kwamba ni
uwanja wa taifa walishangaa kwa namna mashabiki walivyojitokeza kwa wingi.
Hii
inamaanisha kwamba Simba ina mtaji mkubwa wa watu ambao wanawazunguka wakiwatumia
vema basi watafikia mafanikio wanayoyafikiria
Kumiliki
uwanja pekee kwa ajili ya mazoezi haitoshi wanapaswa wawe na uwanja wao pia kwa
ajili ya mechi kubwa kama ilivyo Azam wao wapo hatua ya mbele kabisa. Kila kitu kinawezekana kama hili la uwanja limepenya basi hata hili la kuwa na uwanja wa maalumu kwa ajili ya mechi linawezekana.
Pia hata Yanga nao wana kazi ya kufanya kufikia malengo yao kwa kuwa tumeona tayari wameanza mchakato kwenye uwanja wao wa Kigamboni kilichobaki ni kumaliza kwa wakati ili mambo yaende sawa na ukubwa wa klabu hizi kongwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment