IMEELEZWA kuwa sababu kubwa iliyomfanya kocha mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi kuandika barua ya kujiuzulu ni kutokana na kutokuwa na mwenendo wa kuridhisha kwenye timu.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, James Kasusura imeeleza kuwa Kocha Mwambusi aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu mnamo tarehe 26/11/2019 kwa maslahi mapana ya timu hiyo.
Amesema kwa sasa bodi ya timu hiyo imekabidhi timu kwa kocha msaidizi Mohamed Kijuso wakati mchakato wa kumtafuta kocha mwingine ukiendelea.
Hadi sasa timu hiyo ikiwa imecheza michezo 12 kwenye ligi kuu msimu huu, imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare michezo mitano, imepoteza michezo sita, imefunga magoli manane, imefungwa mabao 19, ina pointi 8 na inakamata nafasi ya 19 juu ya Singida United ambao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 7.
.
.
“Bodi inamshukuru mwalimu Juma Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitaji ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo”, amesema Kasusura.
0 COMMENTS:
Post a Comment