UONGOZI wa
Azam FC umesema kuwa leo watapambana mbele ya JKT Tanzania ili kuendeleza ubabe
wao ndani ya ligi baada ya kushinda mabao 5-0 huku Obrey Chirwa akifunga
hatt-rick mbele ya Alliance mchezo wao uliopita.
Azam FC
itashuka kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi kumenyana na JKT Tanzania
ambayo ina kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-2 na Yanga.
Akizungumza
na Saleh Jembe, kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wana imani ya
kufanya vizuri kwenye mchezo wao kutokana na wachezaji kupata morali kubwa.
“Wachezaji
wanajua kazi yao na ushindi tulioupata mbele ya Alliance bado unatupa hali ya
kujiamini zaidi tuna imani tutafanya vema kikubwa sapoti,” amesema.
Abdalah
Mohamed 'Bares' kocha wa JKT Tanzania amesema kuwa wataonyesha kwa vitendo wakiwa
uwanjani kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment