December 5, 2019


PATRICK Aussems amesema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomfelisha kufanya vizuri msimu huu kwenye michuano ya kimataifa ni kuwakosa wachezaji wake muhimu aliowataka wabaki ndani ya kikosi cha Simba.

Aussems kwa sasa sio kocha tena wa Simba baada ya kufungashiwa virago vyake jumla,amesema kuwa hakuwa na mapendekezo ya wachezaji wengi wapya ndani ya Simba na badala yake alipendekeza wale waliofanya vizuri wabaki jambo ambalo halikufanywa na viongozi wa Simba.

"Wakati naondoka kwenda Ubelgiji niliacha ripoti na nilipendekeza Francis Kahata asajiliwe huku Emanuel Okwi na James Kotei nilihitaji waongezewe mkataba nilishangaa kukuta tayari wameachwa na wamepata timu nyingine.

"Ilikuwa ngumu kwangu kufanya vizuri kwani nilikuwa na mshambuliaji asilia mmoja tu ambaye ni Meddie Kagere jambo lililosababisha tushindwe kufanya vizuri mbele ya UD do Songo," amesema.

Simba msimu huu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imeishia hatua ya awali baada ya kutolewa na UD do Songo kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Taifa.

1 COMMENTS:

  1. Hana lolote aache blah blah kule Msumbiji wale wamakonde wao wenyewe walikuwa wanajishangaa kama kweli walikuwa wanacheza na Simba yenyewe hasa au Simba B? Kwani timu nzima ilikuwa ya hovyo kamwe haikuwa mapungufu ya mchezaji mmoja mmoja na kama UD Songo si hofu yakuwa labda walikuwa wanacheza na timu kubwa na wangejiamini basi Simba angechezea hata goli sita safi kabisa hazina utata nenda kaangalie video bado zimo mitandaoni lakini la kushangaza zaidi Beno kakolanya ndie kwa kiasi kikubwa alikuwa Shujaa wa Simba kule Msumbiji lakini Ausems alivyorudi Bongo kamsahau.Manula mzuri ndio ila kwanini umbadilishe kipa aliefanya vizuri?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic