December 22, 2019


Unaambiwa kwa sasa ukiwa ni miongoni mwa kikosi cha Simba, kwa maana ya mchezaji au upo ndani ya benchi la ufundi, lazima ujitambue kwelikweli linapokuja suala la nidhamu.

Hiyo ni falsafa aliyoanza nayo kocha mpya wa kikosi hicho, Sven Vanderbroeck raia wa Ubelgiji ambaye alianza kazi ya kusimamia mazoezi rasmi Desemba 13, mwaka huu.

Sven ameajiriwa baada ya uongozi wa timu hiyo kumtimua Patrick Aussems ambaye naye alikuwa Mbelgiji kwa madai ya wachezaji kumzoea na kusababisha ashindwe kusimamia kwa umakini suala la nidhamu.

Simba Alhamisi ya wiki hii imeingia kambini Dege Beach, Mbweni, Dar wakijiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Kikizungumza na Championi Jumamosi, chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kilisema kuwa, Vanderbroeck amewataka mastaa wa timu hiyo kuhakikisha wanazingatia nidhamu ya kuwahi kwa kila jambo litakalokuwa limepangwa.

“Jamaa anaonekana kuingia kikosini akiwa na sheria ngumu sana na amekuwa akilizingatia na sasa kila jambo linaenda anavyotaka.

“Siku ya kwanza tu baada ya kuanza mazoezi na kikosi aliwataka wachezaji kuhakikisha wanazingatia suala la kuwahi kwa kila program huku akiweka bayana kabisa kuwa hatakuwa na lelemama kwa atakaye onekana hatii suala hilo.

“Mbali na hilo pia Vanderbroeck anaonekana kuwa na misimamo mikali hasa linapokuja suala la nidhamu kwani hata alipotanganza kikosi kuingia kambini hiyo juzi Alhamisi alionekana akiwasisitiza zaidi kuwahi na akasema kati ya vitu ambavyo hatavivumilia ni suala la mtu kukiuka makubaliano yake,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ili azungumzie ishu huu simu yake iliita bila kupokelewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic