NOVEMBA
haijawa sawa kwa baadhi ya makocha wengi hapa Bongo tumeona pia hata nje huko
nako mambo yalikuwa vurugu mechi.
Tunaona kwa
sasa mashabiki wa Arsenal meno nje baada
ya kocha wao aliyedumu kwa muda wa miezi 18 Unai Emery kupingwa chini baada ya
kupewa mikoba ya Arsene Wenger.
Huko balaa
lake tuachane nalo kwa kuwa mambo yao wanayajua wenyewe na mwezi Novemba tayari
umeshameguka tupo kwenye mwezi mwingine wa Desemba sasa ni muda wa kujipanga
upya kujua wapi tulikosea.
Kwenye
upande wetu sasa Ligi Kuu Bara ambapo bado ipo mzunguko wa kwanza tunaona
kwamba makocha wengi wameachishwa kazi zao na sasa timu zitakuwa chini ya
makocha wengine wasaidizi ama wale waliopewa mkataba.
Kwa sasa habari
kubwa ni kocha wa Simba Patrick Aussems kusimamishwa jumla na uongozi wa Simba
licha ya kuifikisha timu hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu
uliopita sio tatizo kuona haya yakitokea kwa timu kubwa ni kawaida.
Sababu kubwa
kila timu inayoajiri kocha inakuwa na malengo na hesabu ambazo kocha anapewa
iwapo atashindwa kuzifuata basi mwisho wake unafika na maisha yanaendelea.
Ukweli ni
kwamba kwa wimbi ambalo limetokea kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi hali
inaonekana kuwa ni mbaya kwa makocha Bongo hapa kuna kitu ambacho kinapaswa
kifanyiwe kazi.
Achana na
Yanga kumfukuza Mwinyi Zahera usisahau kwamba hata Alliance FC nao walimfukuza
Athuman Bilal ‘Bilo’ baada ya kusimamia mechi moja sawa na dakika tisini na
alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mbao FC.
Kuna jambo
ambalo halipo sawa kwa uongozi wa timu zetu Bongo ama ndani ya mfumo mzima wa
timu zetu hasa kwenye utawala na kama huu mwanya hautazibwa mapema basi msimu
huu makocha wemgi watasimamishwa kazi.
Timu
zinataka matokeo huo ni ukweli tena yale mazuri lakini kuna vitu ambavyo
vinachangia hayo matokeo kupatikana ndani ya uwanja na nje ya uwanja kikubwa ni
kuwa na mipango thabiti na makini kwa timu kiujumla.
Matokeo
yakiwa mabaya makocha wanapigwa chini hilo lipo wazi lakini wale ambao ni
wahusika wakubwa wa matokeo wamekuwa wakiwaachia mzigo wa lawama makocha huu ni
uonevu wa haki unapaswa upingwe kwenye timu zetu zote Bongo.
Utashangaa kwa
mwendo ambao unakwenda kwa sasa hata
Azam FC na Mbao pia nao watampiga chini kocha wao kwa kuwa umeshakuwa ni mtindo
kwa timu zetu zikiona hakuna matokeo basi zinakimbilia kuwatimua makocha.
Msingi
mkubwa wa makocha unajengwa na falsafa zao ambazo wanazisimamia pamoja na
kufanya kazi kwa ushirikiano jambo ambalo linawafanya wapate matokeo chanya
uwanjani.
Kuna mengi
ya kufanya kabala ya kumpiga chini jumla kocha ambaye anafanya kazi na timu
hasa kama amekaa muda mrefu kwa kuwa utambulisho mpya unaleta masuala mapya
ambayo yanaweza kuwa magumu kwa kocha anayekuja.
Kila kocha
ana mbinu zake na mipango yake anayosimamia kuifikikisha timu anapotaka je
katika misingi anayopitia hakukuwa na
mirija yoyote ambayo ilikuwa imekatwa na kuzuia ule mfumo wake kuwafikia walaji
kwa uhakika?
Ni ngumu
kuikataa hali ya makocha kutimuliwa maisha ya soka wakati mwingine yanayumbishwa
na ule upepo ambao unakuwa kwenye soka wakati huo jambo la msingi kujiuliza ni
maamuzi sahihi yanafanywa ama mtu mmoja tu amejiskia na kufanya mambo hayo?
Yote kwa
yote makocha ambao wanapewa majukumu yao kuyasimamia nao wanapaswa wazingatie weledi
wa kazi kwa kufanya kile ambacho wanakiamini kitawapa matokeo bila kugawa
makundi na kugawa timu.
Tuwe
wavumilivu katika mapito magumu ambayo tunapitia hasa kwetu sisi ambao
tunahitaji mafanikio ya haraka hakuna kitu kama hicho kwenye soka kila kitu ni
mipango na mbinu ambazo zinapangwa.
Gharama
kubwa zinatumika kwa makocha kutimuliwa ambazo zingetumika kulipa masuala
mengine ya msingi ambayo yanapaswa yaendelee kufanyika ndani ya timu kwa maendeleo
ya taifa.
Kuna masuala
ya malipo kwa wachezaji, posho na masuala mengine ya msingi ambayo yangeweza
kutumia zile gharama za malipo kwa makocha wetu ambao wanafukuzwa jumla.
Tupunguze
kukurupuka katika maamuzi iwapo tunaona yatatugharimu busara na hekima wakati
mwingine zinapaswa zitumike kupata kile ambacho tunakihitaji licha ya kwamba
tutatumia muda mrefu.
Tufanye
maamuzi sahihi wakati sahihi iwapo tumekubali nakuridhishwa kwamba
tunachokwenda kukifanya kipo sawa na hakuna ambaye amekurupuka katika kufanya
masuala hayo ya maamuzi.
Viongozi
wasifanye haraka katika kuwasimamisha na kuwafukuza makocha wanapaswa watafute
suluhisho mapema kabla ya kufikia hatua ya kumfukuza kocha ambayo ni hatua ya
mwisho kabisa.
Viongozi
watazame vitu muhimu vya kufanya na kuwapa majukumu yanayostahili makocha
ambayo wana imani kwamba watayatimiza kwa wakati bila kuboronga.
Nawaomba
viongozi wawe makini katika kila hatua kwani wao ndio wanaongoza timu ambazo
zinawapa furaha mashabiki suala la maumivu hakuna anayefikiria ila matokeo ya
mpira huwezi kuyazuia.
Kocha
anaajiliwa kwa kufukuzwa hilo lipo wazi lakini muda mwingine inapaswa
kuangaliwa wakati gani anafukuzwa na amefanya nini ndani ya timu.
Iwapo vile
ambavyo alifanya ni vibaya basi ni haki yake kufukuzwa na kuambiwa ukweli kwamba
alikosea sehemu fulani kabla ya kuanza kumlamu kwa kushindwa kwakwe.
Kwa mambo
ambayo yalikuwa kwenye mkataba kwamba iwapo atashindwa kuyafikia basi mlango wa
kutoka utakuwa wazi anapaswa afungashiwe virago ila kama haikuwa sehemu ya
makubaliano na masuala ya kuvunja mkataba ni wakati wa viongozi kutulia na
kufanya maamzui sahihi.







Itoe arsenal katika mifano yako,usifananishe arsenal na hizi takataka za bongomuvi
ReplyDelete