JOSE Mourinho, kocha mkuu wa Totthenham amesema kuwa wachezaji wake waliidharau timu ya Manchester United jambo lililosababisha wakafungwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Manchester United yote mawili yalifungwa na mshambuliaji wao Marcus Rashford ambapo moja alifunga kwa shuti kali na lile la pili alifunga kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezwewa rafu ndani ya 18.
Bao pekee la kufutia machozi kwa Totthenham lilifungwa na Dele Alli halikuweza kuwasaidia kuwapa pointi tatu muhimu wakiwa ugenini.
Mourinho ambaye amewahi kuifundisha Manchester United, amesema kuwa aliwaambia wachezaji wake kwamba wanapaswa waiheshimu Manchester United kwani itakuwa nyumbani licha ya kushindwa kupata matokeo mazuri mbele ya Bournermouth ,Sheffield United na Aston Villa mechi zao za hivi karibuni,
"Tulijua kwamba kuna jambo gumu la kufanya kwenye mchezo wetu na kila mchezaji nilimwambia hilo na tulikuwa na njaa ya ushindi mwisho wa siku tumepoteza, labda imetokana na kujiamini kupita kiasi hili ni funzo kwetu,".
Matokeo hayo yanaishusha Spurs kutoka nafasi ya tano mpaka ya nane ikiwa na jumla ya pointi 20 baada ya kucheza mechi 15 huku United ikipanda mpaka nafasi ya sita kutoka nafasi ya 10 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 15.








0 COMMENTS:
Post a Comment