December 11, 2019


Kocha mtarajiwa wa Simba, Mzambia Beston Chambeshi amesema kwamba ndani ya siku mbili zijazo atakuwa Dar es Salaam kusaini mkataba na klabu hiyo. Lakini Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ameliambia Spoti Xtra Jumamosi iliyopita kwamba;

“Mpaka sasa makocha 72 wameomba kazi, ndio tunaendelea kuwachekecha.” Chambeshi ambae kwa sasa anaikochi Nkana, alikuwa Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Simba kisha akarejea kwao na wamemwambia kesho au keshokutwa atakuja kumaliza ishu.

 Licha ya Simba kufanya siri kubwa kuanzia ujio wa kocha huyo mpaka kuondoka kwake, lakini gazeti la Spoti Xtra lilikuwa la kwanza kushtukia ishu hiyo na kuiripoti na mwenyewe akakiri. Kocha huyo anayependa soka la pasi na nguvu, wakati anakuja nchini Jumatano aliwazuga Nkana kwamba amechoka, anataka kupumzika wiki mbili, hivyo wampe ruhusa kidogo.

“Nimesharudi Zambia kwa sababu waliniita kwa ajili ya mazungumzo, siyo kusaini mkataba, lakini nakuja huko katika siku mbili zijazo, yaani Jumatatu au Jumanne nitakuwa huko kwa ajili ya kusaini kisha kazi ianze mara moja kutokana na mechi kubwa iliopo mbele yao,” alisema Chambeshi ambaye ni Kocha wa Mtanzania, Hassan Kessy anayekipiga Nkana.

“Najua watacheza na Yanga, sasa kila kitu kikienda sawa basi haitokuwa shida kwa sababu najua ndio wapinzani wa jadi wa Simba, nawajua vizuri kwa kuwa nimekuwa niwafuatilia, suala la matokeo nadhani nikishakuwa huko nitawaeleza,” alisema Chambeshi ambaye anaifundisha pia timu ya vijana ya Zambia.

CHANZO: SPOTI XTRA

4 COMMENTS:

  1. Khaa tumechoka na hizi stories za huyu kocha.Unajua mwandishi unajidhalilisha na hizi habari fake za huyu kocha kuja Simba.kila kukicha ni chambeshi kuwa kocha mkuu mpya wa simba. umemng'ang'ania kama luba

    ReplyDelete
  2. Hahahahaha Mmekazaniaaa na Chambeshi wenuu
    Haya ss yamewashukaaa

    ReplyDelete
  3. Huyo mpeleke yanga ndio timu yako tuache salehe tafadhali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic