December 9, 2019


Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umewataka mabosi wa Yanga kufuata taratibu husika ili kumalizana na Kocha wake, Mecky Maxime.

Siku chache zilizopita Yanga wamekuwa wakielezwa kuwania saini ya Mexime ambaye amekuwa na mwenendo mzuri ndani ya Kagera ili aje kuwa Kocha Msaizidi.

Taarifa kutoka Kagera zinasema kuwa moja ya kigogo kutoka klabuni hapo amewaonya Yanga kuacha harakati za kutaka kumchukua kocha wao kwa njia ambazo si sahihi na badala yake wafuate taratibu.

Ameeleza kuwa si vibaya Yanga kuhitaji huduma yake lakini akiwaambia kuwa bado wana mkataba naye, hivyo kama wanamhitaji vema wakafuata taratibu rasmi.

2 COMMENTS:

  1. Watani wameelemewa na mengi pamoja na nyota wao kutaka kuondoka Kwa kutolipwa stahiki zao na ndio wamekuwa wakifanya ya ajabu bila ya malengo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie mna malengo gani mmekuwa kama walemavu maana kila kitu anafanya mliyemuuzia timu yenu bwana mo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic