TIMU yetu ya
Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ipo nchini Uganda ambapo inaendelea
kupeperusha bendera kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Tumeona
ilianza kwa kichapo mbele ya Kenya kwa kuchwapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ufunguzi ikiwa ni fundisho na somo kwa wachezaji ambao wanawakilisha taifa
letu ambalo linazidi kutafuta mafanikio ya soka hasa kwa wakati huu ambao soka
linazidi kukua.
Kila mmoja
anapenda kuona timu inashinda jambo ambalo kila mmoja anapenda kuanzia benchi la
ufundi mpaka wachezaji hesabu zao ni kushinda.
Kupoteza
mchezo wa kwanza haikuwa na maana kwamba hawana uwezo na hawafai hali hii hutokea kwa mashabiki pale ambapo timu inaboronga hii ni mbaya kwa
mashabiki kununa.
Bado kuna
muda wa kujipanga na kuweza kuonyesha kwamba tunaweza kuwa na nguvu kwa ukanda
wa Afrika Mashariki kwani safari moja huanzisha nyingine.
Tukumbuke
kwamba kwa sasa tayari Kilimanjaro imetinga hatua ya nusu Fainali ya michuano hiyo licha ya kuanza kwa kusuasua kwani haikumaanisha kwamba hesabu zimewagomea Kilimanjaro kufanya vizuri.
Ushindi wa bao 1-0 mbele ya Zanzibar uliwarudidha kwenye chati kwani waliweza kumudu kuulinda ushindi wao na ndugu zao ambao walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Sudan.
Mpira hauna
matokeo ambayo watu wanayatarajia ila ni yale ambayo yanapatikana ndani ya
uwanja kushindwa, kushinda na kutoa sare ndio maana ya mpira wenyewe.
Hakuna haja
ya kuzungumza sana kuhusu matokeo yao mabovu ila tunapaswa tuangalie namna gani
timu itakuwa inapata matokeo chanya kwenye mechi zinazofuata kwa kuwa hatuwezi kubadili
matokeo ambayo yameshatokea uwanjani.
Bado timu
itabaki kuwa yetu watanzania hata tukiwasema haiwezi kubadili maana zaidi ya
kuwashusha morali yao tukubali kwamba wachezaji wanajituma matokeo yatakuja.
Suala la
sapoti ni kitu cha msingi kwa timu yetu ambayo inafanya kazi kwa ajili ya taifa
kiujumla na kuachana na maneno ambayo hayaleti matokeo chanya kwa timu yetu.
Pia kumekuwa
na malalamiko kuhusu kikosi ambacho kinapangwa hasa kwenye mechi ya kwanza ambapo wengi
wanalaumu kwa nini Aishi Manula alicheza hana uwezo wanadai wao, sio sawa.
Wengine wanauliza
kuhusu Juma Kaseja kuachwa Bongo wakidai kwamba ni makusudi ama nafasi yake
ilibidi ibaki mkononi mwake wasisahau kwamba ile ni timu ya taifa sio timu ya
mtu mmoja kwa sasa.
Benchi la
ufundi lina matakwa yao ambayo wanaamini yakitendewa kazi yataleta manufaa
suala la kumchagua nani awe ndani ya kikosi liachwe chini ya benchi la ufundi.
Kila mmoja
akiwa kocha basi itakuwa mvurugano kwenye soka letu la ndani ambalo bado
halijafikia hatua ambayo kila mmoja anafikiria liweze kufika nina imani kukiwa
na subira matunda yake tutayaona.
Tujivunie
vya kwetu tuwape sapoti muda wote bila kuchoka na bila kujali aina ya matokeo
yanayotokea hawa ni vijana na wanawakilisha taifa letu pendwa tusisahau hilo
katka vichwa vyetu.
Maisha ya
soka yanaendelea kila siku na ushindani unakua kila iitwapo leo kutokana na
kukua kwa teknolojia na wale ambao wanapenda soka.
Tusisahau
kwamba michuano ina ushindani mkubwa na kila mmoja anahitaji ushindi. Imani
yangu ni kwamba timu yetu ina kila sababu za kuongeza juhudi na kuonyesha ubora
wao katika mechi ambazo zimebaki.
Naona timu
itakuja kutengamaa na kufanya mambo makubwa ambayo bado mashabiki hamjafikiria
kuyaona kwa kuwa mmeanza kukata tamaa mapema.
Kila mmoja
asisahau kwamba kushindwa kwa Kilimanjaro haimaanishi watashindwa siku zote
mwanzo unachangamoto zake na kwa kuwa wameanza kupata hasira watakuwa katika
hali bora mechi zinazofuata.
Kwa sasa
michuano inaendelea tusiwavunje moyo vijana hawa tuwafariji na tusisahau
kuwaombea dua wafanye vema mwisho ili waushangaze ulimwengu.
Hawa
wachezaji wetu ndio ambao wanacheza kila siku tukianza kuwabeza mapema
tutawapotezea nguvu yao ya kutafuta mafaniko ambayo ipo kwenye vichwa vyao.
Kila mmoja awe
na mapezi ya kweli ndani ya moyo wake jambo ambalo litawafanya wajihisi wana deni
kubwa mara mbili zaidi ya walilonalo kwa sasa.
Kwa sasa
mambo bado kwa kuwa kazi inaendelea kwa wale wenye uwezo mkubwa wasisahau
kufika nchini Uganda kuipa sapoti timu na kuwapa moyo vijana bila kuchoka.
Bado kuna
kazi ya kufanya kwa ajili ya kulikuza soka letu kwani wahenga walisema mwanzo ni
mgumu na kuwa mashindano yanaendelea vijana wasituagushe wafanye kweli kwenye
mechi zao zilizobaki.
Kila mchezaji awe na uchungu na taifa lake na
apambane kuona kwamba anapata matokeo chanya licha ya kwamba wameanza mchezo wa
kwanza kwa kuboronga.
0 COMMENTS:
Post a Comment