December 5, 2019


JURGEN Klopp, kocha wa Liverpool amesema kuwa mabao mawili yaliyofungwa na Divock Origi yanafurahisha kuyatazama kutokana na ubora wake.

Liverpool ilishinda mbele ya Everton kwa jumla ya mabao 5-2 jambo linalozidi kuwaweka kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Klopp amesema kuwa mabao yote yaliyofungwa kwenye mchezo huo yalikuwa bora na kila mmoja alifanya kazi yake ipasavyo. 


"Nilitazama namna Origi alivyokuwa akigusa mpira na kufunga ilikuwa inafurahisha kwa namna anavyojiamini, Ila yote kwa yote ni ushindi mzuri tumepata jambo la kufurahisha," amesema.

Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe jumla ya pointi 43 baada ya kucheza mechi 15, haijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Manchester United huku wapinzani wake wakubwa Manchester City wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao 32 tofauti ya pointi 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic