December 8, 2019

JURGEN Klopp, kocha mkuu wa Liverpool amesema kuwa hamchukii mshambuliaji wake Mohamed Salah raia wa Misri ila ni maamuzi yake kutomtumia kwenye kikosi chake kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu.

Klopp hakuwatumia nyota wake wawili ambao ni Salah na Robert Firmino kwenye mchezo wa Ligi Kuu England alioshinda kwa mabao 5-2 dhidi ya Everton uwanja wa Anfield wote walianzia benchi kwenye ushindi huo uliomuweka matatani kocha wa Everton, Marco Silva ambaye kwa sasa ameshafukuzwa kazi ndani ya kikosi hicho cha Everton.

Klopp amesema kuwa anawapenda wachezaji wake wote aliamua kuwapumzisha kwani kuna michezo mingi ya kucheza kutokana na ratiba kuwabana jambo lililomlazimisha afanye mabadiliko ya kikosi chake cha Kwanza.

Klopp amesema kuwa wachezaji wake sio mashine ama wachezaji wa ndani ya gemu "PlayStation' wanahitaji mapumziko wakati ukifika watatumika bila wasiwasi.


Liverpool inaongoza Ligi Kuu England ikiwa na pointi zake 46 baada ya kucheza mechi 16, haijapoteza mchezo mpaka sasa zaidi ya kuambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Manchester United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic