UONGOZI wa
KMC umewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo juu ya afya ya Mohamed Samatta ambaye alipata majeruhi kwenye mchezo wa dhidi ya
Yanga.
Samatta
aliumia mguu baada ya kuchezwa rafu na nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi na
kumfanya mwamuzi Elly Sasi kumuonyesha kadi ya njano Tshishimbi.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa mashabiki
wasiwe na mashaka na Samatta kwani hana maumivu makubwa anaendelea vizuri.
“Samatta
alipata majeraha ya kawaida tu kwani licha ya kushindwa kuendelea na mchezo
alipewa huduma ya kwanza na sasa anaendelea vizuri, wachezaji wamepewa
mapumziko atarejea uwanjani timu ikirudi kambini,” amesema Binde.
KMC imevunja
uteja na Yanga ambayo msimu uliopita ilikomba pointi zote sita za ligi kwa
kuifunga KMC nje ndani kwenye mechi zilizochezwa uwanja wa taifa baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1.







0 COMMENTS:
Post a Comment