Hassan Mwakinyo bondia wa ngumi za kulipwa Bongo amemaliza tofauti zake na bondia mstaafu Rashid Matumla kutokana na tofauti zao za muda kwa kile ambacho Mwakinyo alidai kuwa Matumla alikosa uzalendo.
Mwakinyo alishinda kwa pointi pambanao lake la hivi karibuni dhidi ya Mfilipino Arnel Timampy na Matumla kuchambua mchezo huo jambo lililomkasirisha Mwakinyo.
Mwakinyo ameamua kuomba msamaha kutokana na kumponda bondia huyo mwenye heshima na mwisho wa siku wamemaliza tofauti zao.
"Sikutegemea kama inaweza kuwa hivi ila nimejifunza na ninahitaji msamaha kwa makosa yangu," amesema Mwakinyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment