LICHA ya nyota wa Manchester City, Raheem Sterling kupachika bao la mapema dakika ya 22 kipindi cha kwanza halikuwapa nafasi City kusepa na pointi tatu mbele ya Newcastle United na kuwafanya City wasiamini wanachokiona.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana ulikuwa na ushindani mkali kwani Newcastle United walitumia dakika tatu kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jetro Willems dakika ya 25.
Kipindi cha pili Manchester City walijihakikishia kusepa na pointi tatu baada ya kupachika bao kali dakika ya 82 kupitia kwa Kevin de Bruyne dakika ya 82 jambo lililowafanya mashabiki waamini wanabeba pointi zao kabla ya Jonjo Shelvey kutibua utamu huo dakika ya 88.
Sare hiyo inawafanya Manchester City kuwa nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 29 huku Newcastle United ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 16 huku kileleni akiwa ni Liverpool mwenye pointi 40.
0 COMMENTS:
Post a Comment