December 11, 2019


Wakati wasanii kibao wakiandika historia kwenye shoo ya Fiesta kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, usiku wa kuamkia leo, staa wa Afro-Pop kutoka Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameweka rekodi nyingine huko Afrika Magharibi katika nchi ya Guinea Bissau na kutamba kukomba ‘minoti’ ya uhakika.

Baada ya kuisimamisha nchi ya Siera Leone hivi karibuni, wikiendi iliyopita ilikuwa ni zamu ya Guinea Bisau ambapo Diamond au Mondi alipata mapokezi ya kifalme ambayo hata yeye mwenyewe yalimshangaza.

“Diamond…Diamond… Simba…Simba…Baba Lao..,” walisikika umati uliokusanyika kumpokea Mondi katika Uwanja wa Ndege wa Guinea Bisau.

“Mamaa…ona…ni kwa jinsi gani watu wa Guinea Bisau wanavyompenda kijana wao..,” Mondi alitupia kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika hivyo.

Kwa mujibu wa mitandao ya nchini humo, Mondi alipata mapokezi ya aina yake na kufuatiwa na shoo ambayo alijaza uwanja wa mpira wa Lino Correia na kulamba mkwanja mnono.

Hata hivyo, baadaye Mondi alitupia picha kwenye Instagram akiwa ameshika na kusambaza noti nyingi kiasi cha kuzikanyaga ambazo zilitajwa kuwa ni pesa za Guinea Bisau ziitwazo Guinea Bisau Franc (Faranga za Guinea Bisau).

Hata hivyo, hakutaja fedha hizo ni kiasi gani.

“Ona…katika nchi ambayo watu wake wanazungumza Kireno, siyo Kingereza wala Kiswahili, siwezi hata kuelezea ninavyojisikia,” alisema Mondi kupitia kipengele cha Insta Story (IS) kwenye ukurasa wake wa Instagram akisindikiza na video ya umauti uliokuwa ukikanyagana ili kumuona.

1 COMMENTS:

  1. Nakukubali sana mdogo wangu kwa kazi kubwa unayoifanya ya kutengeneza mkwanja na kulitangaza taifa letu kupitia kazi yako ya muziki,lakini naomba jitahidi kubadilika......punguza ushamba,wapo wnamuziki wengine wengi wa tanzania nao wanajitahidi kutengeneza hela na wengine walianza kuzitengeneza kabla yako lakini hatujawahi kuona wakifanya mbwembwe za kuonyeha fedha zao.....najua unaweza kusema au baadhi ya mashabiki wanaweza kusema kuwa mbona kuna wanamuziki wengine wakubwa wa ulaya wanafanya hivyo.....ni sawa lakini huo sio ustaarabu wetu sisi watanzania kufanya vitendo kama hivyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic