December 8, 2019


JAMIE Vardy nyota wa Leicester City ni moto wa kuotea mbali ndani ya Ligi Kuu England kwa kutupia kwani amewaacha mbali nyota waliotwaa kiatu cha dhahabu msimu uliopita.

Msimu uliopita, Pierre Aubameyang wa Arsenal, Sadio Mane na Mohamed Salah wote wa Liverpool waliibuka na tuzo ya kiatu bora baada ya kufunga mabao 22.

Vardy kwa sasa akiwa amecheza dakika 1350 amefunga jumla ya mabao 14  ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 96 na ametoa asisti 3.

Aubameyang amecheza dakika 1350 amefunga jumla ya mabao 10 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 135 hana asisti huku Mane akitupia jumla ya mabao 9 na asisti nne.

Salah amecheza jumla ya dakika 1103 amefunga mabao 7 na asisti nne. Timu zote zimecheza jumla ya mechi 16 jambo linaloongeza utamu kwenye vita ya kiatu cha mfungaji bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic