December 27, 2019


Washindwe wenyewe sasa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Simba juzi Jumatano kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Katika mchezo huo ambao mashabiki wa Simba walipewa zawadi ya Krismasi na timu yao hiyo pendwa, ulitengeneza njia nyeupe kwa Simba kuelekea kuutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara waliouchukua mara mbili mfululizo kutokana na ratiba kuwa rafi ki zaidi kwao kuliko watani zao wa jadi, Yanga.

Simba ilianza kujipatia bao lake la kwanza kupitia kwa Francis Kahata aliyefunga dakika ya 10 akimaliza pasi ya Shomary Kapombe. Dakika ya 49, Meddie Kagere aliongeza bao la pili akiunganisha pasi ya Clatous Chama.

Hassan Dilunga akafunga kwa penalti dakika ya 57, kisha Dilunga akafunga hesabu dakika ya 64 baada ya kupokea pasi safi  kutoka kwa Sharaf Shiboub.

Kwa sasa njia ya ubingwa kwa Simba ni nyeupe kwani wapinzani wao wa jadi, Yanga ambao wamekuwa wakitamba kwamba watawaharibia, juzi Jumanne walisuluhu na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine ambao walikuja kuulalamikia kwamba haukuwa rafi ki kwao.

Sasa kesho Ijumaa tena Yanga itakuwa Sokoine kucheza na Prisons, kama mambo yakiwa vilevile vibaya, basi Simba itazidi kuwaacha mbali sana kwani hivi sasa mabingwa hao watetezi wapo kileleni na pointi zao 28.

Yanga inazo 18. Tofauti yao ni pointi kumi ambapo Simba imecheza mechi 11 na Yanga 9. Ikumbukwe kuwa, timu hizo zitakuja kupambana Januari 4, mwakani, lakini kabla ya kukutana, Simba itakuwa na michezo miwili jijini Dar ambayo itacheza kwenye uwanja saaafi  usiokuwa na visingizo vya kukosa matokeo, huku Yanga ikiwa na mechi moja Mbeya kwenye uwanja korofi , kisha nyingine Uwanja wa Uhuru ambao upo katika hali nzuri. Simba itacheza na KMC na Ndanda, huku Yanga ikicheza na Prisons na Biashara United.


3 COMMENTS:

  1. Mechi 38 nyie mnazungumza ubingwa hata nusu ya mzunguko wa raundi ya kwanza haujaisha hebu acheni kupumbaza jamii

    ReplyDelete
  2. Weka wazi unakusudia nini kwa msemo wako huo. Kwani hujui siku njema na mbaya inajulikana toka asubuhi?

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu ungesoma vizuri kwani tofauti ya mechi mbili (2) ndiyo kigezo anachoongelea na kumbuka timu zenye ushindani ni hizi za Yanga na Simba tu. Ulitaka aandike nini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic